Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Hawza ya Wasichana ya Hazrat Zainab (as) iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam, imeandaa kikao maalumu cha khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kuwaombea Mashahidi wa Vita vya Ramadhan, akiwemo Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei.

Kikao hicho kilifanyika Jumatatu, tarehe 6 Julai 2026 (20 Muharram 1447 H), kwa ushiriki wa wanafunzi 144 wa Hawza hiyo pamoja na wasimamizi wao, Washiriki (hao) walisoma Qur'an Tukufu na kumuomba Mwenyezi Mungu Awajaalie Mashahidi hao rehema, msamaha na daraja ya juu Peponi.

Waandaaji wa shughuli hiyo walieleza kuwa lengo la khitma hiyo ni kuenzi mchango wa Mashahidi katika kuutumikia Uislamu, kuimarisha utamaduni wa kushikamana na Qur'an Tukufu, na kuwaombea amani na umoja Waislamu duniani.


Your Comment